Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Aweso, Luku ya Maji Kuletwa Tanzania

Waziri wa Maji na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Pangani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Juma Aweso, ametangaza ujio wa mfumo mpya wa malipo ya huduma ya maji utakaofahamika kama “LUKU ya Maji”, ambapo wananchi watapata huduma hiyo kwa kiwango cha fedha watakachoweka kwenye mita zao.

Aweso ameutaja mpango huo mbele ya Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika Kinyerezi, Ilala – Dar es Salaam, ambapo amesema mfumo huu utampa mwananchi uwezo wa kudhibiti matumizi ya maji kulingana na uwezo wake kifedha, kama ilivyo kwa mfumo wa umeme wa LUKU.

Aweso aliongeza kuwa ujio wa mfumo huo ni matokeo ya maono na uongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuboresha sekta ya maji ili kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa Watanzania.

Mpango huu wa "LUKU ya Maji" unatarajiwa kuanza kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa serikali wa kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa ufanisi, haki na uwazi kwa kila Mtanzania.

 

Chanzo: Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: