Aliyekuwa Katibu Mtendaji wa CHADEMA mkoa wa Mwanza Bw. Boniface Mkoba, ameamua mwenyewe bila kulazimishwa kuachana na chama hicho na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, mbele ya mkutano wa kampeni za Urais kupitia CCM katika uwanja wa Nyamagana mkoani Mwanza leo tarehe 8 Oktoba 2025.
Bw. Boniface amejiunga na CCM na kusema ametimiza ndoto yake ya kuchana na chama cha kuhamisha vurugu na kuhamia chama chenye kubeba matarajio ya watanzania katika maendeleo.
Chanzo; Clouds Media