“Kuikosoa serikali sio kosa , kumkosoa Rais Samia Suluhu si kosa’’. Kiongozi wa chama cha Upinzani Tanzania John Heche ameitaka serikali ya nchi hiyo kuelezea alipo aliyekuwa balozi wa nchi hiyo huko Cuba Humphrey Polepole. Shutuma ambazo mamlaka zimekanusha
Jeshi la polisi nchini Tanzania kwa upande wake limeambia BBC kuwa limeanzisha rasmi uchunguzi wa tuhuma za kutekwa kwa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kama zilivyotolewa na familia yake.
Chanzo; Bbc