Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

CCM, ACT wasaini maridhiano ya kisasa

Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo leo Julai 9, 2026, wamesaini Waraka wa Pamoja wa Maridhiano ya Kisiasa kwa lengo la kupata suluhu ya changamoto zilizojitokeza baada ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, hali iliyosababisha Chama cha Upinzani kutoshiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Baada ya takribani miezi sita ya kutokuwepo kwa ushiriki wa ACT-Wazalendo katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa, Vyama hivyo viwili vimefikia hatua hiyo muhimu ya kusaini waraka wa maridhiano unaolenga kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa masuala mbalimbali yenye maslahi kwa Taifa na Wananchi wa Zanzibar.

Waraka huo wa pamoja uliwasilishwa na Katibu wa Kamati ya Maridhiano ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mansura Mosi Kassim ikiwa ni hatua ya pili ya mchakato wa mazungumzo ya maridhiano unaoendelea kati ya pande hizo mbili.

Kuhusiana na mada hii: