Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwanaharakati Chadema Aunt Lulu Apinga Vikali Maandamano

Mwanaharakati wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni muigizaji wa filamu nchini, Lulu Mapunda, ametoa wito kwa wanaharakati wenzake walioko nje ya nchi kusitisha juhudi za kuhamasisha maandamano katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga, Lulu amesema ni muhimu kuwapa nafasi Watanzania kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi bila vuguvugu lolote la maandamano ambalo linaweza kusababisha taharuki.

Nawaomba wanaharakati wenzangu walioko nje ya nchi tusubiri uchaguzi upite kwanza. Tukishaona matokeo na hali ya kisiasa imetulia, ndipo tufanye maandamano ya amani kudai katiba mpya na masuala mengine ya msingi,” amesema Lulu.

Ameongeza kuwa amani na utulivu wakati wa uchaguzi ni muhimu zaidi kwa maendeleo ya taifa, akisisitiza kuwa mabadiliko ya kweli hupatikana kwa njia ya kidemokrasia na siyo kwa vurugu.

 

Chanzo: Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: