Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

KUHUSU EBOLA TANZANIA IPO SALAMA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania kwa sasa ipo salama dhidi ya mlipuko wa virusi vya Ebola, huku akisisitiza kuendelea kuchukuliwa kwa hatua za tahadhari hususan mipakani.

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo Juni 4, 2026 Bungeni Jijini Dodoma, baada ya kuulizwa swali na Mbunge wa Viti Maalum, Asha Salum Moto.

Moto: Hivi karibuni kumeibuka taarifa ya kuenea kwa ugonjwa wa Ebola katika Nchi jirani, je Serikali imejipangaje kudhibiti na kukabiliana na janga hilo?

Waziri Mkuu: Kwanza nitumie Bunge lako tukufu kusema mpaka sasa Nchi yetu ipo salama, ni jambo la kumshukuru Mungu.

Tanzania si kisiwa, Serikali inaendelea kutoa elimu na kuliomba Bunge kuendelea kupaza sauti juu ya tahadhari, pamoja na Watanzania wote kuchukua tahadhari.

Pia tuwe na utayari, Mtu anapotoka Nje ya Nchi awe Mtanzania au si Mtanzania afanyiwe vipimo na tuwe tayari kutokuficha tetesi wala dalili zozote.

 

 

Kuhusiana na mada hii: