Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Putin Awataka Vijana Duniani Kutimiza Ndoto Zao Kupitia Urusi

 

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amewakaribisha washiriki na wageni wa Tamasha la Kimataifa la Vijana (International Youth Festival), akisema vijana wana nafasi muhimu katika kuunda mustakabali wa dunia huku maendeleo ya teknolojia yakiendelea kubadilisha maisha ya binadamu.

Akizungumza kupitia ujumbe maalum kwa washiriki wa tamasha hilo linalofanyika Yekaterinburg, mji uliopo kati ya Ulaya na Asia, Putin alisema eneo la Urals limekuwa kitovu cha mageuzi makubwa ya viwanda, sayansi na maendeleo ya Urusi kwa karne nyingi.

Putin alisema Yekaterinburg ni mahali sahihi kwa viongozi vijana kutoka mataifa mbalimbali kukutana na kujadili namna teknolojia mpya zinavyobadilisha maisha ya watu na aina ya dunia wanayotaka kuijenga katika siku zijazo.

Rais huyo alisisitiza umuhimu wa urafiki, amani na maelewano kati ya mataifa, akieleza kuwa neno la Kirusi “mir” lina maana ya amani, urafiki na dunia kwa ujumla, jambo ambalo alisema linaakisi misingi ya taifa la Urusi.

“Tunataka kila mtu aendelee kuwa binadamu na maisha yake yasiamuliwe na utaifa wake, utajiri, hadhi au historia yake. Tunaamini kila taifa lina haki ya kuchagua njia yake ya maendeleo kwa uhuru,” alisema Putin.

Aidha, alieleza kuwa mataifa yote yanapaswa kuwa na fursa sawa ya kupata huduma muhimu kama dawa, chakula, maji, nishati, elimu pamoja na teknolojia za kisasa ambazo zinapaswa kupatikana kwa manufaa ya binadamu wote.

Putin aliwahimiza vijana kushirikiana katika kujenga dunia iliyo wazi, yenye haki na inayojumuisha kila mtu, akisema Urusi iko tayari kuwakaribisha wale watakaotaka kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo.

“Nina hakika kizazi cha vijana kitafanikiwa. Huu ni wakati wenu. Fuateni ndoto zenu pamoja na Urusi,” alisema.

Tamasha la Kimataifa la Vijana limekusanya maelfu ya vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani kujadili masuala ya maendeleo, teknolojia, uongozi, ubunifu na ushirikiano wa kimataifa.

Kuhusiana na mada hii: