Washiriki kutoka Tanzania wanaohudhuria Mkutano wa 63 wa Shirikisho la Kimataifa la Polisi Wanawake (IAWP) Nchini Indonesia wameahidi kutumia kikamilifu maarifa na uzoefu watakaoupata katika mkutano huo kwa lengo la kuboresha huduma wanazozitoa kwa Wananchi Nchini Tanzania.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Eda Mkisi amesema Jeshi la Polisi pamoja na Washiriki wengine kutoka Tanzania wamejipanga kujifunza kutoka kwa Mataifa mbalimbali yanayoshiriki mkutano huo ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.
Amesema mkutano huo umefungua fursa kubwa ya kukutana na Wataalamu na Wawakilishi kutoka Nchi mbalimbali duniani jambo ambalo litawawezesha kujifunza mbinu na uzoefu mbalimbali unaoweza kutumika kuboresha huduma za Jeshi la Polisi nchini Tanzania.
Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Mariam Kobero, amesema sekta ya utalii kama moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya fedha za kigeni nchini Tanzania huku akiweka wazi kuwa kwa umuhimu huo wataendelea kupata mafunzo ndani na nje ili kuboresha huduma za uhifadhi Nchini Tanzania.
Askari wa Tanzania Washiriki ufunguzi IAWP Indonesia
- Chanzo:
- Millard Ayo