Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Akaunti Bandia Zilivyovamia Mitandao ya Kijamii

Kadri matumizi ya mitandao ya kijamii yanavyozidi kuongezeka, ndivyo changamoto mpya za kidijitali zinavyoibuka, ikiwemo matumizi ya akaunti bandia maarufu kama bots, ambazo zimeanza kutawala mijadala mingi, kwa lengo la kushawishi au kupotosha maoni ya umma.

Ingawa suala la bots si geni duniani, nchini Tanzania tatizo hilo limeshika kasi kwa sasa, hasa kuanzia kipindi cha Uchaguzi Mkuu, ambapo mijadala mitandaoni ilijaa hashtag kama #OktobaTunatiki na #NoReformsNoElection.

Bots hutengenezwa mahsusi kusambaza ujumbe fulani mara nyingi, ili kuunda taswira ya uungwaji mkono mpana, hali inayoweza kuwapotosha watumiaji wa mitandao hiyo.

Athari za matumizi ya bots ni pana, zikiwemo kupotosha mjadala wa umma, kueneza taarifa zisizo sahihi pamoja na taarifa za uongo zinazotolewa kwa makusudi sambamba na kuchochea migawanyiko au taharuki katika jamii.

Jinsi ya kuzitambua
Akaunti nyingi za bot huonekana kwa kuangalia kwa makini taarifa za ‘profaili’ za wahusika. Mara nyingi hutumia majina yasiyo na utambulisho binafsi mfano John Smith2024 au Africa Voice, bila picha halisi ya mtu, bali hutumia picha za jumla zilizopakuliwa mtandaoni.

Akaunti hizo pia huwa na wafuasi wachache au hufuata akaunti nyingine nyingi zinazofanana kimuundo na kimaudhui, hali inayoashiria ni mtandao wa akaunti bandia unaoendeshwa kwa lengo moja mahsusi.

Mbali na profaili, mienendo ya akaunti hizo huibua mashaka, ikiwemo kuchapisha ujumbe mara kwa mara ndani ya muda mfupi bila kupumzika, mara nyingi kwa kutumia maneno yale yale kwenye mijadala tofauti.

 

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: