2025, kama ilivyokuwa miaka iliyopita, nenosiri "123456" limeibuka tena kuwa nenosiri lililotumika zaidi duniani kote.
Ripoti ya kila mwaka kutoka NordPass ambao kila mwaka wanaachia 200 bora ya password zilizotumika imethibitisha kuwa mamilioni ya watumiaji bado wanategemea mfululizo huu rahisi wa nambari, licha ya maonyo mengi kutoka wataalamu.
Huko U.S watumia wengi wanatumia neno la siri linalo shahabiana ambapo 123456, 12345678, 123456789 ni top 3 ya password zilizotumiwa zaidi nchini humo.
Zaidi, Password hizo zinatumiwa na watu wa lika wakiwemo Gen Z ambao wanaonekana ni familia ya kidijitali ijapokuwa wataalamu upiga marufuku utumiaji wa password hizo mfuatano kwani ni rahisi kudukuliwa.
Chanzo: Tanzania Journal