Video zaidi ya laki tano kutoka nchini Kenya zafutwa na Tiktok kwa kukiuka kanunua za mtandao huo, kwa mujibu wa ripoti ya tiktok ya robo ya pili ya mwaka 2025.
Ambapo, kuna kanuni za Jamii za TikTok “Community Guidelines” zaidi ya 20 maalum ambazo zikivunjwa au usipozifata zinaweza kusababisha video yako au maudhui yako yote kufutwa mara moja, kupunguziwa mwonekano, au akaunti yako kufungiwa.
Zikiwemo zile za Afya ya akili na tabia, usalama na ustahimivu ambazo zinagusia mambo ya unyanyasaji wa kijinsia, uhalifu na chuki, nyingine ni ile ya maudhui ya wakubwa.
Chanzo; Tanzania Journal