Windows 11 sasa haitaruhusu tena watumiaji kutumia mfumo huo bila kuwa na akaunti ya barua pepe.
Awali, watumiaji waliweza kuanza kutumia Windows kwa kuunda local account bila kujisajili mtandaoni.
Hata hivyo, Microsoft imetangaza kuondoa kabisa njia ya bypass kwenye hatua ya Out of Box Experience (OOBE). Hii ina maana kwamba kila mtumiaji atalazimika kuingia au kujisajili kwa kutumia akaunti ya barua pepe wakati wa usakinishaji wa mfumo.
Hatua hii inalenga kuimarisha usalama na kurahisisha huduma za mtandaoni, lakini pia inalazimisha watumiaji wote kuwa na akaunti ya Microsoft.
Chanzo: Mwananchi Scoop