Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Google Inakuruhusu Kubadilisha Gmail Sasa

Baada ya miaka zaidi ya 20 tangu Gmail ianzishwe, Google sasa imeanza kuwaruhusu watumiaji kubadilisha barua pepe zao za @gmail.com kuwa nyingine mpya inayoishia @gmail.com.

Kipengele hiki kimeanza kuenezwa polepole kwa watumiaji wote duniani kote, na kwa sasa kimeonekana zaidi India (kwenye kurasa za msaada kwa lugha ya Kihindi).

Unapobadilisha barua pepe yako ya zamani kuwa mpya, ile ya zamani itabaki kama jina la ziada: Barua pepe zitakazotumwa kwenye ya zamani zitafika kwenye kisanduku chako kimoja, na unaweza kuingia kwenye akaunti yako kwa kutumia yoyote kati ya hizo mbili.

Vitu vyote uliyo navyo kama barua pepe za zamani, picha, faili kwenye Google Drive, na mengineyo vitabaki salama bila kupotea.

Masharti muhimu,
- Baada ya kubadilisha, huwezi kubadilisha tena barua pepe mpya kwa miezi 12.
- Unaweza kubadilisha barua pepe mara 3 tu kwa akaunti moja (yaani jumla ya barua pepe 4).

Kipengele hiki bado kinaenezwa hatua kwa hatua, kwa hivyo huenda kisipatikane kwa kila mtu sasa hivi. Ili kuangalia kama umepata, nenda kwenye mipangilio ya akaunti yako ya Google (Personal info > Email).


Chanzo: Tanzania Journal

Kuhusiana na mada hii: