Kampuni ya Norinco ya China kwa msaada wa jeshi la nchi hiyo imetengeneza roboti za mbwa vita wanaoweza kushiriki mapambano katika uwanja wa vita.
China inajaribu kutumia robot dogs na makundi mengine ya droni yanayoweza kushambulia kwa pamoja.
China pia imezindua gari la kijeshi linalojiendesha kwa akili bandia ya DeepSeek. Gari hilo lina uwezo wa kufanya kazi za kivita bila dereva.
Faida yake ni kuongeza kasi na usahihi katika vita.
Hata hivyo, hatari ni matumizi ya silaha zisizo na udhibiti wa binadamu na migongano ya kimaadili.
Chanzo: Global Publishers