Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Selcom Business yazinduliwa rasmi na kubadili sura ya Malipo ya Kidijitali kwa Biashara Tanzania

Katika hatua inayotarajiwa kuongeza kasi ya matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali nchini, Selcom Microfinance Bank imezindua Selcom Business, akaunti mpya ya benki ya kidijitali inayolenga kuwapa wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs), kampuni na watengenezaji wa mifumo (developers) huduma za benki zenye gharama nafuu, uunganishaji wa mifumo kwa haraka na usimamizi bora wa fedha za biashara.

 

Uzinduzi huo unakuja wakati ambapo biashara nyingi nchini zinaendelea kutafuta njia za kupunguza gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi kupitia teknolojia. Selcom Microfinance Bank inaeleza kuwa huduma hiyo imebuniwa kushughulikia changamoto mbili zinazowakabili wafanyabiashara wengi—gharama kubwa za kufanya miamala na muda mrefu unaochukuliwa kuunganisha mifumo yao na taasisi za kifedha.

Kupitia Selcom Business, biashara zinaweza kufanya uhamisho wa fedha kwenda benki zote za ndani, mitandao ya simu na wafanyabiashara wanaotumia TanQR kwa gharama ya kuanzia TZS 100 kwa kila muamala. Vilevile, biashara zinaweza kujisajili na kupata REST APIs moja kwa moja kupitia dashboard ndani ya saa chache, bila kulazimika kupitia taratibu ndefu za makubaliano au kulipa ada za uunganishaji wa mifumo.

Benki hiyo imeeleza kuwa hakuna kikomo cha idadi ya miamala inayoweza kufanywa ndani ya mwezi. Kadri biashara inavyochagua bando kubwa zaidi, ndivyo gharama ya kila muamala inavyopungua. Viwango vyote vinajumuisha VAT na ushuru wa bidhaa.

Ubunifu Unaolenga Kuongeza Ufanisi wa Biashara
Mbali na gharama nafuu za miamala, Selcom Business imejengwa juu ya huduma tatu kuu ambazo benki inaamini zitabadilisha namna biashara zinavyofanya shughuli zao za kifedha.

Kwanza ni bei nafuu za miamala, ambapo biashara zinaweza kufanya uhamisho wa fedha kwa gharama ya kuanzia TZS 100 kwa kila muamala kupitia Bando Max bila kikomo cha idadi ya miamala ndani ya mwezi.

Pili ni API za kujihudumia, zinazowawezesha wafanyabiashara kupata API credentials, kuweka IP whitelist, callback URLs na kusimamia ukwasi (liquidity) kupitia dashboard bila kusubiri taratibu za muda mrefu za uidhinishaji. Mfumo huo unapatikana kupitia REST APIs kwa huduma za usimamizi wa akaunti, malipo, uhamisho wa fedha na makusanyo kupitia Lipa Number.

Tatu ni udhibiti wa matumizi ya fedha za biashara, ambapo waajiri wanaweza kufanya malipo ya mishahara, malipo ya makundi na matumizi ya petty cash kwa hatua tatu tu. Mfumo pia una ufuatiliaji wa matumizi kwa wakati halisi, stakabadhi za kidijitali na viwango tofauti vya ruhusa kwa watumiaji kulingana na majukumu yao.

Kuhusiana na mada hii: