Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Dhahabu Yapanda Bei Marekani, Wawekezaji Watafuta Usalama Kuweka pesaa

Bei ya dhahabu imefikia rekodi ya juu ya zaidi ya $4,000 (£2,985), huku wawekezaji wakitafuta maeneo salama ya kuweka pesa zao kutokana na wasiwasi kuhusu kutokuwa na uhakika wa kiuchumi na kisiasa kote ulimwenguni.

Gharama ya dhahabu imeshuhudia kupanda zaidi tangu miaka ya 1970, ikipanda kwa zaidi ya 25% tangu Aprili wakati Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza ushuru ambao umevuruga biashara ya kimataifa.

Wachambuzi wanasema suala jingine linalowatia wasiwasi wawekezaji ni kuchelewa kutolewa kwa data muhimu za kiuchumi kutokana na kufungwa kwa serikali ya Marekani, huku ikitarajiwa kuingia wiki yake ya pili.

Dhahabu inaonekana kama kinachojulikana kama uwekezaji wa mahali salama, ambao unatarajiwa kuhifadhi au kuongeza thamani yake wakati wa misukosuko ya soko au kuzorota kwa uchumi.

Bei ya dhahabu safi, kiasi unachopokea ukiuza madini hayo ya thamani kwenye kaunta, ilipanda zaidi ya $4,011 kwa ounce moja Jumatano asubuhi huko Asia.

Kufungwa kwa serikali ya Marekani, ambako kulichochewa na msukosuko wa mara kwa mara juu ya matumizi ya umma, ni "kinyume cha bei ya dhahabu", alisema Christopher Wong wa OCBC, ambaye ni mtaalamu wa mikakati wa benki hiyo yenye makao yake makuu Singapore.

Wawekezaji wamegeukia mali salama kama dhahabu wakati wa kufungwa kwa serikali ya Marekani hapo awali.

 

Chanzo; Bbc 

Kuhusiana na mada hii: