Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bandari za Bukoba, Kemondo Kuchochea Uchumi Kanda ya Ziwa

Mradi wa Maboresho na Upanuzi wa Bandari ya Bukoba pamoja na Kemondo, mkoani Kagera kwa gharama ya Sh39.8 bilioni, umekamilika kwa asilimia 100.

Kukamilika kwa maboresho na upanuzi wa bandari za Bukoba na Kemondo imeelezwa kuwa kutachochea ukuaji wa uchumi mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Mkazi wa Mradi, Mnanka Maginga amesema mradi katika bandari zote mbili umekamilika kwa kiwango kikubwa na hivyo kurahisisha shughuli za utekelezaji.

Maofisa wa Bandari wa Bukoba na Kemondo, Ismail Malick na Mohamed Mayoro, wameeleza kuwa mradi huo umefungua fursa mpya za kiuchumi na usafiri wa mizigo na abiria kupitia Ziwa Victoria.

Wananchi wa Mkoa wa Kagera nao wameishukuru Serikali kwa uwekezaji huu muhimu unaotarajiwa kuchochea ukuaji wa biashara, ajira na maendeleo ya kijamii katika ukanda wa ziwa.

Kwa sasa, shughuli zote za utekelezaji na uendeshaji zinaendelea kwa ubora na ufanisi, hali inayodhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya bandari nchini.

 

Chanzo: Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: