Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

China Kuongeza Kodi Kwenye kondom

Katika kutekeleza mkakati wa kuhamasisha familia kupata watoto nchini China Serikali ya nchi hiyo imesema itaongeza kodi ya thamani (VAT) ya asilimia 13 kwa bidhaa za dawa na vifaa vya uzazi wa mpango ikiwemo Kondom ambazo zitaondolewa katika Orodha ya bidhaa zisizokuwa na kodi.

China imefikia uamuzi huo kutokana na kuwepo kwa kiwango kidogo cha jumla ya uzazi nchini humo huku idadi ya watoto ikiwa chini ya asilimia 50 kwa muda wa muongo mmoja huku idadi ya vijana ikiendelea kupungua kwa kasi kitendo kinachotishia upatikanaji wa nguvu kazi ya taifa na uzalishaji kupungua kitendo kinachopelekea ukuaji wa mda mrefu kuwa hatarini.

Aidha Kwa upande wa wataalamu wanaeleza kuwa kuna hofu kubwa kupandishwa huko kwa bei ya kondomu na vifaa vingine vya uzazi wa mpango kunaweza kuongeza mimba zisizotarajiwa na kusababisha ongezeko la maambukizi ya magonjwa ya zinaa

Hata hivyo bado haijafahamika kama njia hiyo itaenda kutatua changamoto hiyo ya upatikanaji wa watoto japo nchi kadhaa kama vile Pakistani iliongeza kodi ya thamani kwa asilimia 17 na kiwango cha uzazi kilikuwa kwa watoto 3.6 kwa kila mwanamke huku Nchini India licha ya Kondom kuwa bure kiwango cha uzazi kimeendelea kushuka kwa kiwango cha watoto 2.0 kwa Mwanamke mmoja.

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: