Data mpya ya idadi ya watu inaonyesha kwamba wanaume ambao hawajawahi kuoa na hawana watoto ni mojawapo ya makundi yanayoongezeka kwa kasi zaidi katika maeneo kama vile Marekani. Wanaume zaidi wanaingia katika umri wa miaka ya 30 na 40 bila kuingia katika majukumu ya kitamaduni kama vile ndoa au kuwa baba.
Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na Kituo cha Pew Research na Psychology Today kwa nyakati tofauti zimebaini kuwa ongezeko hilo limetokana na shinikizo la kifedha, maamuzi binafsi ya mtu, kupanda kwa gharama za maisha, kuwekeza nguvu nyingi kufikia malengo binafsi na wakati mwingine kwa sababu tu hawajakutana na mwanamke sahihi anayefaa (Mwenzi).
Wataalamu wameongeza kuwa mabadiliko haya yanatokana na mchanganyiko wa mitazamo inayobadilika kuelekea mahusiano, kuamua kuzingatia kazi, matamanio ya kuishi maisha ya uhuru wa mtu binafsi. Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kwamba wengi wa wanaume hao hawapingani na wazo la ndoa au kuwa na watoto wanafuata ratiba tofauti na vizazi vilivyopita.
Chanzo; Crown Media